Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha mpango wa Marekani wa kusitisha mapigano unaojumuisha uwepo wa majeshi ya uvamizi huko Ghaza kwa jina la vikosi vya uthabiti wa kimataifa.
Hamas imekataa uwepo wa wanajeshi wa kigeni Ghaza na imesema haitobadili ukaliaji wa mabavu wa Israel kwa “uvamizi wa kigeni”.
Wakati wa kupitishwa kwa maazimio hayo, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni katika shule moja katika kitongoji cha Daraj, jijini Ghaza, yaliwajeruhi Wapalestina wapatao 13 wakiwemo watoto. Maafisa wa Ghaza wanasema kuwa; Wapalestina waliokimbia makazi yao wanahitaji mahema yapatayo 300,000 kwa ajili ya makazi, kwani Ghaza inakabiliwa na msimu wa baridi kali sana unaokuja.
Vita vya Israel dhidi ya Ghaza tangia Oktoba 2023 hadi sasa vimewaua Wapalestina wapatao 69,483 na kujeruhi au kuwalemaza 170,706.
Chanzo: Nukuu kutoka Shirika la Habari la Al Jazeera
Maoni yako